• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Libya akanusha kuomba kikosi cha kulinda amani cha UM

    (GMT+08:00) 2018-10-02 10:31:58

    Waziri wa mambo ya nje wa Libya Bw. Mohamed Sayala amekanusha kuomba mabadiliko ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya kutoka ya kisiasa hadi ya kikosi cha kulinda amani, na kueleza kuwa ni muhimu kuigeuza tume hiyo kutoka tume maalumu ya kisiasa hadi tume ya kuunga mkono kuanzishwa kwa usalama na utulivu kote nchini Libya.

    Akihutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumamosi iliyopita, Bw. Sayala pia amesema ushiriki wa Umoja wa Mataifa unapaswa kuwa wa ufanisi zaidi na kuhusika moja kwa moja kwenye mgogoro wa Libya, ukiwemo wa kiusalama, na kuifanya kuwa kipaumbele kuendana na njia ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako