• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: URA kupoteza shilingi bilioni 30 kila mwezi kutokana na sera mpya ya uagiziaji magari

    (GMT+08:00) 2018-10-02 19:05:54

    Mamlaka ya Ushuru ya Uganda (URA) itapoteza shilingi bilioni 30 kila mwezi kufuatia kuanza kutekelezwa kwa marufuku ya magri makuukuu yaliotengenezwa zaidi ya miaka 15 iliyopita.

    Lakini magari yalionunuliwa kabla ya Julai 1 2018 hayataathiriwa na hatua hiyo.

    Kamishena wa forodha kwenye URA, Bw Dicksons Collins Kateshumbwa, amesema magari yaliyoagizwa kabla ya Septemba 30 pia yataruhusiwa nchini.

    Kateshumbwa amesema tarehe ya mwisho imefika na sheria itaanza kutekelezwa.

    Uganda hukusanya kwa wastani shilingi bilioni 120 kutoka kwa uagiziaji wa magari 4,000 mengi yakiwa ni yale yaliuotumika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako