• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yahitaji dola bilioni 4.5 kusambaza umeme

    (GMT+08:00) 2018-10-02 19:06:19

    Uganda itahitaji dola bilioni 4.5 kuwekeza kwenye usambazaji na ugawaji wa kawi ndani ya kipindi cha miaka 10 ijayo.

    Wizara ya fedha nchini humo imesema kati ya fedha hizo dola bilioni 3.5 zitatumika kuweka nyaya za umeme.

    Fedha hizo pia zitatumika kwenye miradi kama vile kukarabati vituo vya zamani vya umeme, kununua transfoma, nyaya na jenereta za dharura.

    Serikali inaendelea kuwekeza kwenye miradi ya kuzalisha kawi huku mabwawa ya Karuma na Isimba ikitarajiwa kufunguliwa mwaka ujao na kuzalisha megawati 783.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako