• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Benki ya Dunia yazuia Sh112 bilioni za msaada

    (GMT+08:00) 2018-10-02 19:09:50

    Benki ya Dunia (WB) imezuia msaada wa Dola milioni 50 kwa Tanzania ikitaka majadiliano zaidi kuhusu mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa kwenye Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015.

    Fedha hizo zilikuwa msaada wa kuisaidia Serikali kuboresha mfumo wa kukusanya, kuchakata na kutunza kumbukumbu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) lakini benki hiyo inaamini kuna vifungu vinavyokandamiza uhuru wa kujieleza.

    Taarifa iliyochapishwa Oktoba Mosi na mtandao wa Eye on Global Transparency' inasema Benki ya Dunia inasikitishwa na ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza na mwenendo wa demokrasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako