• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Mataifa asisitiza umuhimu wa maendeleo shirikishi ya kijamii

    (GMT+08:00) 2018-10-03 10:11:05

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kiuchumi na kijamii Bw. Liu Zhenmin amesisitiza umuhimu wa maendeleo shirikishi ya kijamii.

    Akiongea kwenye ufunguzi wa kamati ya tatu ya Kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Liu amesema kuhakikisha maendeleo shirikishi ya kijamii ni muhimu katika kukamilisha Ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, na hali ya kutokuwa na usawa pamoja na changamoto zinazozikabili ushirikishi wa kijamii zitatatuliwa kwa sera kuhusu fedha, mishahara na ulinzi wa kijamii.

    Pia amesisitiza umuhimu wa kushughulikia mambo yanayohusiana na vijana, wazee, watu wenye ulemavu, familia na wenyeji wa kiasili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako