• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Polisi nchini Scotland waanza uchunguzi kubaini shabiki aliyemjeruhi mwamuzi

    (GMT+08:00) 2018-10-03 10:35:20

    Polisi nchini Scotland wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini shabiki aliyerusha kitu kinachodhaniwa kuwa ni sarafu kilichomjeruhi mwamuzi msaidizi aitwaye Calum Spence siku ya jumatatu kwenye mechi ya ligi kuu.

    Tukio hilo lilitokea mnamo dakika ya 15 ya kipindi cha pili kwenye mechi katika mechi ambayo wakiwa nyumbani Livingstone FC ilipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Glasgow Rangers.

    Chama cha soka cha nchi hiyo kupitia Rais wake Ian Maxwell kimekemea kitendo hicho na kusema hatua za kisheria zitachukuliwa ili kukomesha vitendo visivyo vya kiuanamichezo.

    Aidha kocha mkuu wa Rangers, Steven Gerard amempa pole mwamuzi huyo, na kueleza masikitiko yake huku akisihi matokeo ya uchunguzi yawekwe bayana, pia akisema hii ni tahadhari juu kuimarishwa kwa usalama wakati wa michezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako