• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaeleza msimamo wake katika suala la wakimbizi

    (GMT+08:00) 2018-10-03 16:58:23

    Balozi wa kudumu wa China katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Yu Jianhua ameeleza msimamo wa China juu ya suala la wakimbizi kwenye mkutano wa 69 wa Kamati ya Utendaji wa Mambo ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa.

    Bw. Yu amesema, China inashikilia mfumo wa pande mbalimbali katika utatuzi wa changamoto hiyo, na inahimiza nchi mbalimbali kubeba majumuku tofauti na kuunga mkono zaidi jitihada za Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja huo na nchi zinazopokea wakimbizi. Pia jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza nguvu zaidi katika kutatua migogoro na umaskini na kutotumia fursa hiyo kama kigezo cha kuingilia mambo ya ndani ya nchi husika.

    Pia amesisitiza kuwa, China imetoa pendekezo la kutatua suala hilo kwa kushauriana, kujenga na kuendeleza kwa pamoja ili kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako