• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bolton asema Marekani itajitoa kwenye makubaliano ya hiari ya Mkataba wa Vienna

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:29:12

    Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Bw. John Bolton amesema Marekani inajitoa kwenye makubaliano ya hiari ya Mkataba wa Vienna juu ya utatuzi wa migogoro.

    Akiongea na wanahabari kwenye Ikulu ya Marekani, Bw. Bolton amesema rais Donald Trump ameamua kuitoa Marekani kwenye makubaliano hayo, kufuatia Palestina kufungua mashtaka dhidi ya Marekani kutokana na hatua yake ya kuhamisha ubalozi kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem.

    Bw. Bolton amesisitiza kuwa Marekani bado ni mwanachama wa Mkataba wa Vienna kuhusu mahusiano ya kidiplomasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako