• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kombe la Shirikisho: Enyimba

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:36:45

    Bao pekee la mshambuliaji Abdelilah Hafidi limeipa ushindi wa ugenini wa 1-0 Raja Casablanca dhidi ya wenyeji, Enyimba International katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika usiku wa jana Jumatano uwanja wa Enyimba International mjini Aba, Nigeria.

    Sasa Raja watakuwa na kazi nyepesi ya kuulinda ushindi wao mwembamba katika mchezo wa marudiano Oktoba 24 mjini Casablanca nchini Morocco ili waingie fainali ya michuano hiyo namba mbili kwa ukubwa barani.

    Katika mchezo mwingine wa nusu fainali ya kwanza uwanja wa Al Masry Club mjini Port Said, wenyeji Al Masry wamelazimishwa sare ya bila kufungana na AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako