• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Federer, Serena kuchuana Hopman Cup

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:37:38

    Mabingwa mara nyingi wa tenisi duniani Serena Williams na Roger Federer ni miongoni mwa wachezaji waliothibitisha kushiriki michuano ya kombe la Hopman.

    Katika michuano yam waka huu Serena Williams ataungana na Frances Tiafoe kuiwakilisha Marekani wakati Federer ataungana na Belinda Bencic kuwakilisha Uswisi, wakitetea ubingwa wao walioutwaa januari mwaka huu.

    Tayari ratiba ya michuano hiyo imetolewa ambapo Serena na Tiafoe watashuka dimbani januari mosi mwakani kucheza dhidi ya Federere na Belinda kwenye uwanja wa ndani wa Perth Arena.

    Mashindano ya Hopman yamebuniwa kwa ajili ya kuwapa wachezaji fursa ya kujiandaa kwa mashindano ya wazi ya Australia yatakayoanza Januari 14 mwakani mjini Melbourne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako