• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania aiagiza Wizara ya mambo ya nje kufanya mageuzi makubwa

    (GMT+08:00) 2018-10-04 09:46:24

    Rais John Magufuli wa Tanzania ameiagiza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya nchi hiyo kufanya mageuzi makubwa yanayolenga kuboresha ufanisi wa mambo ya kidiplomasia.

    Rais Magufuli amesema hayo katika Ikulu ya Dar es Salaam, wakati alipomuapisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Fariji Kasidi Mnyepe, akisisitiza kuwa mageuzi hayo yanatakiwa kutatua changamoto zinazoikabili wizara hiyo.

    Rais Magufuli pia amesema baadhi ya maofisa kwenye wizara hiyo wamefanya vizuri lakini wengine hawana uwezo wa kutosha kwa kuwa wamekaa madarakani kwa muda mrefu kupita kiasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako