Waziri wa fedha wa Russia Bw. Anton Siluanov amesema mpango wa kuondoa dola za kimarekani kwenye uchumi wa Russia umeandaliwa na kuwasilishwa kwa serikali.
Bw. Siluanov amesema mpango huo unawataka wauzaji nje kutumia ruble ya Russia badala ya dola ya kimarekani kwenye miamala ifikapo mwaka 2024.
Msemaji wa Ikulu ya Russia Bw. Dmitry Peskov amesema mchakato wa kuondoa dola za kimarekani kwenye uchumi wa Russia ni mgumu na utachukua muda mrefu, na hakuna mipango ya kuacha kabisa matumizi ya dola za kimarekani kwenye miamala.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |