• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya NMB Tanzania yazindua wiki ya huduma kwa wateja

    (GMT+08:00) 2018-10-05 18:58:23

    Benki ya NMB imezindua wiki ya huduma kwa wateja huku ikijikita katika kuendeleza huduma zake kidigitali.

    Wiki ya huduma kwa wateja ambayo huazimishwa Oktoba kote duniani inalenga kuboresha huduma za taasisi mbalimbali kwa wateja wao.

    Akizungumza na radio China kimataifa, kaimu mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna amesema benki hiyo imedhamiria kusogeza huduma kwa wateja wake kwa kutumia mtandao ili kurahisisha upatikanaji wake.

    Hivi sasa amesema wana kitengo maalumu cha ubunifu kwa hiyo wataendelea kuja na bidhaa na huduma mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wateja wao.

    Amesema kupitia njia ya simu mteja anaweza kufungua akaunti pamoja na kufanya shughuli mbalimbali ikiwamo kuomba mikopo kwa haraka zaidi.

    Amewataka watoa huduma wa benki hiyo kutoa huduma kwa kuzingatia weledi ili kuendana na kauli mbiu isemayo "Excellence Happens Here".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako