• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watuhumiwa watatu wa mauaji ya raia wa Chini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakamatwa

    (GMT+08:00) 2018-10-07 18:45:08

    Ubalozi wa China nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR umethibitisha kuwa, jana usiku watuhumiwa wakuu watatu wa mauaji ya raia watatu wa China nchini humo wamekamatwa.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya ndani ya CAR Bw. Henri Wanzet Linguissara, washukiwa watatu hao walikamatwa jumamosi usiku na kwamba msako mwingine ungeanza usiku huo huo, na akisema kuwa hatua za kisheria zitafunguliwa mapema.

    Spika wa bunge la nchi hiyo Abdoul Karim Meckassoua jana alitembelea ubalozi wa China nchini humo ambapo alieleza kusikitishwa sana na mauaji ya wahalifu hao, pia alitoa salamu za pole kwa familia za wahanga wa mauaji hayo.

    Kwa upande wake balozi wa China nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Bw. Chen Dong amemhakikishia Spika Meckassoua kwamba ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika una historia ndefu, na hakuna atakayeweza kusimamisha hatua imara zilizopigwa na pande hizo mbili katika kuelekea ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja.

    Aidha Rais wa CAR Faustin Touadera na waziri mkuu wa CAR Simpince Sarandji, wamekutana pia na Balozi wa China, na kutoa salamu za pole huku wakilaani mauaji hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako