• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Magari: Mwingereza Hamilton ashinda Japan, aukaribia ubingwa wa Jumla

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:13:34

    Dereva Lewis Hamilton wa Uingereza sasa amekaribia kushinda ubingwa wa mwaka huu wa mashindano ya magari ya mwendokasi kufuatia ushindi aliopata jana kwenye mbio za Japan mjini Suzuka.

    Kutokana na ushindi wa jana, Hamilton sasa amefikisha alama 331, na ni ushindi wake wa 9 katika mbio 17 zilizokwishafanyika mpaka hivi sasa, akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Sebastian Vettel aliyejikusanyia alama za jumla 264 akiwa ameshinda mara 5 katika msimu huu.

    Katika mbio za jana, Valterri Botas wa Finland alishinda nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Max Verstappen wa Uholanzi.

    Madereva hao sasa wanajianda na mbio za 18 zitakazofanyika Oktoba 21 nchini Marekani, na endapo Hamilton atashinda moja kwa moja atatawazwa kuwa bingwa wa msimu huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako