• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapigano na askari wa Israel yawajeruhi wapalestina 29 huko Gaza

    (GMT+08:00) 2018-10-09 08:15:17

    Wapalestina zaidi ya 29 wamejeruhiwa katika mapigano kati ya maelfu ya waandamanaji na askari wa Israel waliowekwa katika mpaka kati ya ukanda wa Gaza kaskazini na Israel.

    Msemaji wa wizara ya afya Gaza Bw. Ashraf al-Qedra amesema kati ya waandamanaji hao 29 waliojeruhiwa, 11 walipigwa risasi na askari wa Israel, na wawili wako katika hali mbaya. Mbali na maandamano ya kila wiki yanayofanyika kila Ijumaa katika ukanda wa Gaza mashariki tangu Machi 30, yanayojulikana kama "Matembezi Makubwa ya Kurudi", tume ya matembezi hayo pia inafanya maandamano katika ukanda wa Gaza kaskazini kila Jumatatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako