• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaanza vibaya mashindano ya Olimpiki 2018 kwa vijana

    (GMT+08:00) 2018-10-09 08:50:09

    Kenya imeanza vibaya mashindano ya vijana ya Olimpiki ya mchezo wa magongo yanayoendelea jijini Buenos Aires nchini Argentina, baada ya kufungwa na Australia kwa alama 7-0.

    Magoli ya Australia yalifungwa na James Collins na Miles Davis, ambao walifunga magoli mawili kila mmoja huku Lain Carr, Allistair Murray na Ben White wakifunga moja kila mmoja.

    Kocha Kevin Lugalia amesema vijana wake wamepata matokeo hayo mabaya kutokana na woga na wasiwasi wakati wa mchuano huo.

    Hii ni mara ya kwanza Kenya inashiriki katika mashindano hayo, na mbali na Australia, Kenya itachuana pia na Canada, India, Bangladesh na Austria.

    Na timu nyingine kutoka Afrika ni Zambia, ambayo nayo ilianza vibaya baada ya kufungwa na Argentina kwa alama 6-2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako