• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Fifa yatangaza majina 30 ya wanaoshindania tuzo ya Ballon D'or

  (GMT+08:00) 2018-10-09 08:51:30

  Nyota wa kimataifa wa Croatia Luka Modric ameorodheshwa tena katika safu ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya FIFA ya mchezaji bora ya Ballon D'or kwa mwaka 2018.

  Wiki chache zilizopita Modric alijishindia tuzo ya mchezaji bora wa mashindano ya kombe la dunia mwaka huu, tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya na tuzo ya mchezaji bora wa dunia.

  Sababu hii inafanya wengi watabiri kuwa huenda akashinda tuzo ya Ballon D'or ambayo kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita ilishikiliwa na Cristiano Ronaldo, pamoja na Lionel Messi.

  Wengine waliotajwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Cristiano Ronaldo wa Juventus, Lionel Messi wa Argentina, Kylian Mbappe wa Ufaransa, Harry Kane wa Uingereza na Luis Suarez wa Uruguay.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako