• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yasisitiza utayari wa kutoa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo yanayodhibitiwa na waasi

    (GMT+08:00) 2018-10-09 09:14:55

    Serikali ya Sudan imesisitiza utayari wake wa kushirikiana na Umoja wa mataifa, katika kutoa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo yanayodhibitiwa na waasi.

    Wiki iliyopita serikali ya Sudan ilisaini makubaliano na Umoja wa mataifa kuhusu kutoa misaada ya kibinadamu na kuanzisha kampeni ya chanjo kwenye maeneo yanayodhibitiwa na kundi la SPLM tawi la kaskazini katika majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini.

    Waziri wa afya wa Sudan Bw. Mohamed Abu Zaid Mustafa amelihimiza kundi hilo kuzingatia maslahi ya raia na kukubali mpango wa Umoja wa mataifa, na pia amesisitiza unyumbufu wa wizara yake katika kutekeleza kampeni hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako