• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia itarahisisha utaratibu wa kuomba visa kwa nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-09 09:37:22

    Rais Mulatu Teshome wa Ethiopia amesema katika muda mfupi ujao, watu kutoka nchi za Afrika wataweza kwenda Ethiopia bila kuhitaji visa kabla. Rais Teshome ameliambia bunge kuwa juhudi sasa zinafanywa kwa wasafiri kutoka nchi za Afrika kuomba visa wanapowasili nchini Ethiopia.

    Rais Teshome amesisitiza kuwa Ethiopia ambayo ni makao makuu ya mashirika kadhaa ya kikanda na kimataifa, imekuwa ikiimarisha juhudi za kuwafanya watu kutoka nchi za Afrika waingie Ethiopia bila visa, hatua ambayo inaendana na pendekezo la Umoja wa Afrika kuhakikisha watu wanasafiri kwa uhuru na kuwa na utaratibu wa kutoa visa wanapowasili kabla ya mwaka 2063.

    Rais Teshome pia amesema mkanganyiko kati ya uhuru na kukosekana kwa sheria, kunachangia sana uharibifu na wako kukosa makazi. Amesema hayo kufuatia matukio yaliyotokea wiki iliyopita katika jimbo la Benishangul Gumuz, na kufanya watu elfu 70 wapoteze makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako