• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yapunguza makadirio ya ongezeko la uchumi wa dunia katika mwaka huu na ujao

    (GMT+08:00) 2018-10-09 19:23:26

    Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limetangaza kupunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia hadi asilimia 3.7 katika mwaka huu na mwaka ujao, huku likionya kuwa ongezeko la wasiwasi wa kibiashara ni tishio kuu linaloukabili uchumi wa dunia.

    Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika hilo imeonesha makadirio ya kasi ya ongezeko la uchumi wa dunia katika mwaka huu na ujao itapungua kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na makadirio yaliyotolewa mwezi wa Julai.

    Shirika hilo limekadiria kuwa mwaka huu kasi ya ongezeko la uchumi wa nchi zilizoendelea ni asilimia 2.4, kasi hiyo kwa Marekani ni asilimia 2.9, eneo linalotumia Euro ni asilimia 2 na Japani ni asilimia 1.1. Kasi ya ongezeko la uchumi wa soko linalojitokeza na nchi zinazoendelea inakadiriwa kuwa asilimia 4.7, huku kasi ya China ikikadiriwa kuwa asilimia 6.6 hivi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako