• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Wakulima 500 waagizwa kuondoka kwenye msitu

  (GMT+08:00) 2018-10-09 19:44:32

  Zaidi ya wakulima 500 wameagizwa kuondoka kwenye msitu wa Bugiri mashariki mwa Uganda.

  Mamlaka ya misitu nchini humo imewapa wakulima hao wa mpunga hadi mwishoni mwa mwaka huu kuondoka.

  Mkaguzi wa mamlaka hiyo katika eneo la Bugiri Betty Nansubuga, amesema eneo hilo ni chepechepe na hivyo ni kinyume cha sheria kuendesha shughuli za kilimo hapo.

  Nansubuga, ameelezea kuwa wakulima hao wamekuwa wakikaidi agizo la kuondoka kwenye eneo hilo wakilalamika kuwa ndio njia ya pekee ya kujiendeleza kiuchumi.

  Mbunge wa eneo hilo Asuman Basalirwa sasa ameiomba serikali kuwatafutia wakulima hao mipango mingine ya kuleta mapato ili kuepusha mzozo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako