• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini ateua waziri mpya wa fedha

    (GMT+08:00) 2018-10-10 09:15:12

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua Bw Tito Mboweni kuwa waziri mpya wa fedha, baada ya mtangulizi wake Bw. Nhlanhla Nene kujiuzulu.

    Bw Mboweni alikuwa Gavana wa Benki Kuu ya Afrika Kusini na waziri wa kazi, na anatajwa kuwa na uzoefu mkubwa kwenye maswala ya fedha, sera za uchumi na utawala bora.

    Kujiuzulu kwa Bw. Nhlanhla kunatokana na kujulikana kuwa na uhusiano na familia ya Gupta, ambayo ina sifa mbaya kuhusu vitendo vya ufisadi nchini Afrika Kusini.

    Huku nyuma Bw. Nhlanhla aliongopa kwa kusema amewahi kukutana na familia ya kina Gupta kwenye sherehe za kitaifa, lakini wiki iliyopita aliomba msamaha na kusema aliwahi kwenda nyumbani kwa kina Gupta mara mbili kati ya mwaka 2010 na 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako