• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania awaondoa madarakani maofisa wanne waandamizi wa polisi

    (GMT+08:00) 2018-10-10 10:07:32

    Rais John Magufuli ametoa amri ya kuwaondoa madarakani maofisa wanne waandamizi wa jeshi la polisi ili kupisha uchunguzi dhidi yao, kuhusu tuhuma za kuhusika na mtandao mkubwa wa biashara ya magendo ya kuvuka mpaka.

    Kurugenzi ya mawasiliano ya rais imetoa taarifa kuwa, maofisa hao ni Augustine Ollomi wa wilaya ya Kagera, Justine Joseph, Robert Marwa na Everist Kivuyo wa Kyerwa. Habari zinasema maofisa hao wametuhumiwa kutoa usindikizaji wa polisi kwa wanaofanya biashara ya magendo ya kahawa na vitu vingine.

    Rais Magufuli pia amewaagiza Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Bw. Jacob Kingu, na Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Simon Siro kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina unafanyika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako