• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na waziri mkuu wa zamani wa Japan na wajumbe wa sekta ya uchumi nchini Japan

    (GMT+08:00) 2018-10-10 17:04:49

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa zamani wa Japan Bw. Fukuda Yasuo na wajumbe wa sekta ya uchumi wa Japan ambao wako China kuhudhuria mazungumzo kati ya wanaviwanda na maofisa wa zamani wa nchi hizo mbili.

    Bw. Wang Yi amesema huu ni mwaka wa 40 tangu China na Japan ziliposaini Makubaliano ya Amani na Urafiki. Amesema nchi hizo zinatakiwa kuimarisha msingi wa kisheria na kisiasa wa uhusiano kati yao, kuthibitisha maoni ya pamoja kuhusu kuchukuliana kuwa mwenzi wa ushirikiano, na kuendeleza uhusiano huo katika siku za baadaye.

    Bw. Fukuda Yasuo amesema, maendeleo tulivu ya uhusiano kati ya Japan na China si kama tu ni muhimu kwa nchi hizo mbili, bali pia ni muhimu kwa kanda ya Asia Mashariki na dunia. Vilevile amesema Japan inapenda kushiriki kwenye mchakato wa mageuzi mapya na kufungua mlango kwa nje nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako