• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yasema Kenya imewaondoa mamilioni ya watu kutoka kwenye umasikini katika mwongo uliopita

    (GMT+08:00) 2018-10-10 18:29:09

    Ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu tathmini ya jinsia na umasikini iliyotolewa jana imesema, idadi ya wananchi wa Kenya wanaoishi chini ya mstari wa umasikini imepungua kidhahiri katika mwongo mmoja uliopita, ingawa mgawanyiko katika nchi hiyo bado unaendelea.

    Ripoti hiyo imesema idadi ya watu wanaoishi chini ya mstari wa kimataifa wa umasikini nchini Kenya imeshuka kutoka asilimia 46.8 mpaka asilimia 36.1 kati ya mwaka 2005 hadi 2015, na hii imetokana na utulivu endelevu wa uchumi.

    Ripoti hiyo pia imeonyesha maendeleo makubwa yaliyopatikana katika maeneo ya vijijini nchini Kenya ambako umasikini umepungua kutoka asilimia 50 mpaka asilimia 38 katika mwongo mmoja uliopita, lakini maendeleo hayakuwa wazi zaidi katika maeneo ya mijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako