• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamia ya wanajeshi wa Ethiopia wafanya maandamano ya kudai nyongeza ya mshahara na marupurupu

    (GMT+08:00) 2018-10-11 08:56:12

    Mamia ya wanajeshi wa Ethiopia jana waliandamana mjini Addis Ababa kulalamikia mishahara midogo na marupurupu, na kuzuia kwa muda barabara inayoelekea kwenye ikulu ya nchi hiyo.

    Mkuu wa Jeshi la Polisi la Ethiopia Bw Zeynu Jemal, amesema wanajeshi wapatao 240 walikuwa na mvutano kiasi na vikosi vya usalama karibu na maeneo ya ikulu ya nchi hiyo. Huduma za simu za mkononi na Internet zilisitishwa kwa muda kutokana na hali ya kukanganya na uvumi kuenea.Wanajeshi hao walitaka kuonana na Waziri Mkuu wa Ethiopia huku wakiwa na silaha zao, lakini baada ya majadiliano, waliruhusiwa kuonana na waziri mkuu bila kuwa na silaha.

    Waziri Mkuu Bw. Abiy Ahmed alifanya mazungumzo na wanajeshi walioandamana na kusikiliza madai yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako