• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watu waliokufa kwenye ajali ya barabarani Kericho, Kenya yafikia 56

  (GMT+08:00) 2018-10-11 10:19:04

  Idadi ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya barabarani iliyotokea jana asubuhi mjini Kericho, Kenya imeongezeka na kufikia 56. Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Kericho Bw. James Mugera amesema idadi hiyo imeongezeka baada ya watu sita waliokuwa wanapatiwa matibabu katika hospitali za Muhoroni na Kericho kufariki dunia.

  Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri, na kati ya wahanga wa ajali hiyo, 15 ni wanawake na wengine 32 ni wanaume, watu 15 wamenusurika.

  Mamlaka ya usafiri na usalama ya Kenya imesema basi hilo, lililokuwa limejaza abiria kupita kiasi lilianguka mteremkoni na kubiringika mara kadhaa. Mmoja wa abiria walionusurika amesema dereva hakuheshimu sheria za usalama barabarani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako