• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa maendeleo ya uchumi usio na uchafuzi wa miji ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" wafanyika

    (GMT+08:00) 2018-10-11 18:28:20

    Mkutano wa tatu wa maendeleo ya uchumi usio na uchafuzi wa mazingira wa miji ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ulioandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa umefanyika huko Vienna nchini Austria, na kuhudhuriwa na wajumbe wa miji 188 kutoka nchi 90.

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong amesema, lengo la mkutano huo ni kuweka jukwaa la kuimarisha uhusiano wa kiwenzi, na kuhimiza kwa pamoja maendeleo endelevu ya viwanda katika miji ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Katika hotuba yake kwa njia ya video, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, ili kujenga miji yenye maendeleo endelevu na ustawi zaidi, sehemu mbalimbali duniani zinafanya ushirikiano, na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ni sehemu muhimu ya ushirikiano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako