• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 8000 wauawa mwaka huu katika mapambano ya kutumia silaha nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-10-11 18:45:53

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan imetoa ripoti mpya ikisema, tangu Januari hadi Septemba, mapambano ya kutumia silaha na mabavu yamesababisha vifo na majeruhi ya raia 8,050 wakiwemo wanawake na watoto, ambao 2,798 kati yao waliuawa na wengine 5,252 walijeruhiwa.

    Ripoti hiyo imesema, vifo na majeruhi vinavyotokana na mapambano bado vinaendelea, na kwamba idadi ya vifo vya raia vilivyotokea katika miezi tisa ya mwanzo imeongezeka ikilinganishwa na ya mwaka jana, ambayo pia ni rekodi ya juu zaidi tangu mwaka 2014.

    Ripoti hiyo pia imesema, mikoa ya Nangarhar, Kabul, Helmand na Faryab imeathiriwa zaidi na mapambano, hasa katika mkoa wa Nangarhar, ambapo raia 1,494 waliuawa katika mapambano kwenye miezi tisa ya mwanzo ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako