• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China awasili Tajikistan kuhudhuria mkutano wa SCO

  (GMT+08:00) 2018-10-11 19:35:12

  Waziri mkuu wa China Li Keqiang amewasili mjini Dushanbe, Tajikistan kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) na kufanya ziara rasmi nchini humo.

  Katika mkutano huo, Bw. Li atajadiliana na viongozi wengine masuala kadhaa ikiwemo kuongeza juhudi zaidi katika kujenga Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kuimarisha ushirikiano katika nyanja kama vile biashara, na mawasiliano ya watu na watu ili kuzidisha ushirikiano wa kivitendo wa Jumuiya hiyo katika maeneo yote.

  Mkutano huo unatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja, kuzungumza kwa sauti moja juu ya masuala makubwa ya kimataifa na kikanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako