• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Afrika wataka hatua madhubuti zichukuliwe kukabiliana na kuongezeka kwa hali joto

    (GMT+08:00) 2018-10-12 08:57:51

    Wataalamu wa Afrika wametoa wito kwa serikali na sekta mbalimbali kuongeza maradufu juhudi za kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni ili kudhibiti kuongezeka kwa hali joto, ambako kumetoa tishio kubwa kwa maisha ya watu na maliasili barani Afrika.

    Wito huo umetolewa kwenye Mkutano wa kilele wa Afrika kuhusu hali ya hewa uliofanyika mjini Nairobi. Wataalamu wamekubaliana kuwa mustakbali wa Afrika unakabiliwa na hatari, kutokana na kuwa kuongezeka kwa hali joto kumeongeza ukame na ukosefu wa chakula, kuleta magonjwa mapya na kuvuruga mfumo wa kiikolojia.

    Mtaalamu kutoka Ethiopia Bw. Yacob Mulugetta amesema kuongezeka kwa joto duniani kutarudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliyopatikana katika nchi za Afrika katika miaka ya karibuni, na kwamba jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kimaadili kuunga mkono juhudi za kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako