• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wazihimiza Sudan na Sudan Kusini zipate maendeleo kwenye suala la mipaka kati yao

    (GMT+08:00) 2018-10-12 18:07:02

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limepitisha azimio na kuongeza muda wa Kikosi cha usalama cha Umoja huo mkoani Abyei kwa nusu ya mwaka hadi tarehe 15 mwezi Aprili mwaka 2019, na kitakuwa na jukumu la kusaidia ukaguzi na utaratibu wa usimamizi wa mipaka ya pamoja kati ya Sudan na Sudan Kusini.

    Azimio hilo linasema, hii ni mara ya mwisho kuongeza muda wa majukumu ya kikosi hicho, isipokuwa kama Sudan na Sudan Kusini zitapata maendeleo kwenye suala la mpaka ndani ya muda huo.

    Abyei ni moja ya sehemu zenye mvutano mkali kati ya Sudan na Sudan Kusini. Mwezi Juni mwaka 2011, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliamua kupeleka kikosi cha usalama mkoani humo, ambacho kilisimamia Sudan na Sudan Kusini kuondoa majeshi yao kutoka sehemu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako