• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madhimisho ya miaka 100 ya Nelson Mandela yafana

    (GMT+08:00) 2018-10-13 16:02:09

    Ubalozi wa Afrika Kusini nchini China umeandaa maonyesho ya kumbukumbu ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa aliyekuwa rais mweusi wa kwanza wa nchi hiyo Nelson Rohihlahla Mandela.

    akifungua maonyesho hayo hapa Beijing, Balozi wa Afrika Kusini Bi. Dolana Msimang amemueleza Mandela kuwa ni shujaa wa dunia kwa vita vyake vya muda mrefu dhidi ya utawala wa Makaburu na ujumbe wake wa Amani na Maridhiano wakati alipoachiwa huru baada ya kutumikia miaka 27 gerezani. Bi Msimang amepongeza juhudi za ushirikiano kati ya Afrika Kusini na China na kuahidi nchi hizo mbili zitaendelea na ushirikiano na kukaribisha makampuni ya China kwenda kuwekeza Afrika Kusini.

    Bidhaa mbalimbali za Afrika Kusini na za China zimeonyeshwa katika maonyesho hayo yaliyohudhuriwa na watu toka mataifa mbalimbali

    Nelsom Mandela aliongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, alizaliwa mwaka 1918 na kufariki mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako