• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya kimataifa ya biashara ya Canton kufunguliwa kesho

    (GMT+08:00) 2018-10-14 16:07:25

    Maonesho ya kimataifa ya biashara ya Canton yatafungliwa kesho mjini Guangzhou nchini China.

    Msemaji wa maonesho hayo Bw. Xu Bing amesema, kampuni 25,583 zikiwemo za nchini China na za kutoka nje zitashiriki kwenye maonesho hayo, na maonesho hayo yataendelea kuweka eneo la bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi nyingine, na kampuni 636 kutoka nchi 34 zitaonesha bidhaa zao kwenye eneo hilo.

    Bw. Xu amesema, hivi sasa asilimia 60 ya kampuni zinazoshiriki kwenye maonesho hayo zinatoka nchi na sehemu za Ukanda Mmoja na Njia Moja.

    Yakiwa dirisha la kufungua mlango wa China kwa nje, Maonesho ya kimataifa ya biashara ya Canton yametoa mchango mkubwa katika kuhimiza uagizaji wa bidhaa kutoka nje na kusafirisha bidhaa kwenda nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako