• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa UN alaani mashambulizi dhidi ya mkutano wa kampenzi za uchaguzi nchini Afghanistani

    (GMT+08:00) 2018-10-14 16:38:05

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani mashambulizi mabaya yaliyotekelezwa dhidi ya mkutano wa kapeni za uchaguzi na dhidi ya ofisi ya moja ya wagombea nchini Afghanistan.

    Akitoa taarifa kwa niaba ya katibu mkuu huyo, msemaji wa Guterres Bw. Stephane Dujarric amesema mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya raia ni uvunjaji wa sheria za haki za binadamu za kimataifa.

    Aidha Bw. Guterres ametoa salamu za pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na kuwatakia kupona majeruhi.

    Katika matukio hayo, vikundi vinavyopingana na serikali vilishambulia watu waliokuwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa wabunge na kuua watu 13 na kujeruhi wengine wengi, na kwingineko ikielezwa kuwa ofisi ya mgombea mmoja katika jimbo la Heart ilishambuliwa na watu wawili wakipoteza maisha akiwemo mtoto na mlinzi wa ofisi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako