• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini yaimarisha utekelezaji wa mageuzi ya ardhi

    (GMT+08:00) 2018-10-15 09:32:17

    Serikali ya Afrika Kusini imesema inaimarisha utekelezaji wa mageuzi ya ardhi ili waafrika kusini waweze kutumia ardhi kwa ajili ya kuboresha maisha yao na kukuza uchumi wa nchi.

    Hayo yamesemwa na rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kwenye sherehe ya kurudishwa ardhi kwa jamii moja ya watu weusi mkoani KwaZulu-Natal. Rais Ramaphosa amesema anaamini kuwa jamii mbalimbali zinapaswa kufuatilia kwa karibu mchakato wa kurudisha ardhi, na pia kushiriki kwenye biashara na shughuli zote kwenye ardhi zao.

    Rais Ramaphosa amesema kukabidhiwa kwa hekta zaidi ya 4,500 za ardhi kwa jamii ya KwaMkhwanazi, kumekuja wakati serikali ya Afrika kusini inafanya juhudi kusahihisha "dhambi ya asili" ya umiliki wa ardhi, na kwamba eneo hilo litakuwa ni sehemu ya ardhi inayolengwa kurudishwa katika miezi michache ijayo.

    Rais Ramaphosa pia ameahidi kuwa serikali itawasaidia wenyeji kuendeleza uwezo wao wa kupata mapato na ajira kutokana na ardhi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako