• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Iran asema nchi hiyo itaweza kujitoa kutoka makubaliano ya kinyuklia ya Iran wakati wowote

    (GMT+08:00) 2018-10-15 18:20:32

    Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema, wakati wowote nchi hiyo inaweza kuchagua kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya Iran kutokana na mahitaji ya maslahi ya taifa na usalama.

    Rais Rouhani amesema hayo alipotoa hotuba katika chuo kikuu cha Tehran. Amesema, serikali ya awamu hii ya Marekani inajaribu kupindua utawala wa sasa wa Iran, na kwamba nchi hiyo imeanzisha vita vya kisaikolojia dhidi ya Iran, na huenda itaanzisha vita vya kibiashara hadi kupindua utawala wa hivi sasa wa Iran.

    Rais Rouhani amesisitiza kuwa kama Iran ikishikamana, itakuwa na uwezo wa kuvunja njama mbalimbali za Marekani kama ilizofanya zamani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako