Korea Kusini na Korea Kaskazini leo zimekubaliana kufanya hafla ya uzinduzi wa mawasiliano ya kisasa na hatimaye kuunga njia za reli na barabara katika mpaka wa nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya majadiliano ya ngazi ya juu yaliyofanyika mapema leo katika Nyumba ya Amani, ambayo ni jengo la Korea Kusini katika kijiji cha Panmunjong.
Kabla ya hafla hiyo iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa Novemba au mwanzoni mwa Disemba, nchi hizo mbili zimekubaliana kufanya utafiti wa njia ya reli kwenye ushoroba wa magharibi wa Peninsula ya Korea kuanzia mwisho wa mwezi huu, na njia ya reli katika ushoroba wa mashariki kuanzia mapema mwezi ujao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |