• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yaahidi kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-10-16 09:01:39

    Naibu rais wa Afrika Kusini Bw. David Makuza amesisitiza ahadi ya nchi yake ya kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini yaliyosainiwa mwezi Septemba na makundi hasimu kwa lengo la kurejesha utulivu nchini humo.

    Bw. Makuza ambaye aliwasili mjini Juba Jumapili kwa ziara ya siku mbili, amefanya mazungumzo na rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, ambapo wamejadili njia za kuhimiza utekelezaji wa makubaliano ya amani.

    Bw. Makuza amewahimiza viongozi na serikali za nchi kwenye kanda hii kushirikiana katika kuunga mkono makubaliano hayo, na pia amedokeza kuwa atakutana na marais wa Uganda, Kenya na Sudan kujadili utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako