• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Charles Mwijage aahidi kuboresha zaidi mazingira ya biashara

    (GMT+08:00) 2018-10-16 19:28:41
    Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Charles Mwijage amesema suala la kuboresha mazingira ya biashara ni maelekezo ya Rais John Magufuli hivyo atajitahidi kuboresha ikiwa ni pamoja na kupunguza mamlaka za usimamizi na kusisitiza kitabu cha mwongozo cha Blue print

    Mwijage amesema hayo wakati akizindua kiwanda cha kuzalisha vilainishi vya mitambo na mashine cha Lake Lubes kilichopo Kigamboni.

    Aidha katika tukio hilo Mwijage amewapigia debe waajiriwa wa kampuni mbalimbali akisema wafanyakazi wanatakiwa kulipwa mishahara minono ili wachagie katika kodi za Serikali kupitia makato ya mishahara na manunuzi wanayofanya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako