Wamesema mafunzo hayo pia yatawasaidia kuanza kuzalisha bidhaa za ngozi za kiwango cha kimataifa.
Wadau kwenye sekta hiyo wamekuwa wakilalamika kuwa ujuzi walio nao ni wa kimsingi tu na hivyo hawawezi kuiendeleza sekta yenyewe.
Mapema mwaka huu baraza la maendeleo ya ngozi lilitaja usimamizi mbaya wa vichinjio kuwa sababu moja ya viwango vya chini vya ngozi.
Licha ya kuwa Kenya ina ngozi ya kutosha lakini makampuni mengi yanaagizia kutoka nje ya nchi kwani kiwango cha nyumbani ni duni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |