• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR ina wasiwasi kuhusu hali ya kibinadamu nchini DRC kutokana na kurudi kwa wakimbizi wengi

    (GMT+08:00) 2018-10-17 09:27:13

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR, limesema lina wasiwasi na hali ya kibinadamu katika jimbo la Kasai, kutokana na kurudi kwa wakimbizi wengi kutoka Angola katika wiki mbili zilizopita.

    Maofisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wamesema wakimbizi laki mbili wamewasili katika jimbo la Kasai peke yake, na wengine wengi wanatarajiwa kuwasili katika jimbo la jirani la Kasai kati. Kurudi kwa wakimbizi hao kunatokana na hatua ya serikali ya Angola kuamua kuwafukuza wageni wanaofanya kazi kiharamu kwenye machimbo, bila kuwaarifu.

    Habari zinasema kumekuwa na mapambano katika baadhi ya maeneo ya Angola, kutokana na idara za usalama kutekeleza amri ya kuwafukuza wageni wanaoishi bila kufuata sheria, baada ya jumatatu ambayo ilikuwa siku ya mwisho iliyowekwa na serikali kwa wageni hao kuondoka, kupita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako