• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afripol yaweka mkazo katika kupambana na ugaidi, uhalifu wa kuvuka mipaka na uhalifu mtandao

    (GMT+08:00) 2018-10-17 09:39:03

    Baraza kuu la Jumuiya ya ushirikiano wa polisi ya Afrika Afripol limeamua kuanzisha vikosi kazi vitatu, vinavyolenga kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka, uhalifu mtandao, ugaidi na itikadi kali.

    Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya amani na usalama Bw. Smail Chergui ametangaza uamuzi huo kwenye kikao cha pili cha Baraza kuu la Afripol kilichofanyika Jumatatu na Jumanne mjini Algiers. Amesema nchi wanachama wa Afripol pia zimekubaliana kufanya mikutano ya Baraza kuu la Afripol kila mwaka, ili kuweka misimamo na mikakati ya pamoja ya Afrika kwenye mkutano wa mwaka wa Polisi ya kimataifa Interpol.

    Bw. Chergui ametangaza kuwa Afripol na Interpol watasaini makubaliano mwezi Januari mwakani, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uratibu kati yao kwenye mapambano dhidi ya ugaidi na uhalifu wa kupangwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako