• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa Marekani asema ni jambo baya kwa tukio la chip za kijasusi kutumiwa kuunga mkono sera za kuipinga China

    (GMT+08:00) 2018-10-17 09:39:43

    Makala mpya iliyotolewa hivi karibu kwenye Jarida la Bloomberg Businessweek, imesema China iliweka chip ndogo kwenye bidhaa za kampuni zaidi ya 30 za Marekani ili kudukua siri. Ripoti hiyo ikakanushwa na kampuni nyingi za Marekani zikiwemo Apple, Amazon na Supermirco kwamba bidhaa zao hazikuwekewa chip na nchi nyingine, na wala hazikutoa ripoti kwa serikali ya Marekani kuhusu tukio hilo. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya usalama wa taifa ya Marekani pia imesema hakuna sababu ya kutilia mashaka taarifa zilizotolewa na kampuni hizo.

    Mtaalamu mashuhuri wa mambo ya kimataifa wa Marekani Bw. Robert Kuhn amesema suala la chip za kijasusi lenyewe si tatizo kubwa, lakini ni jambo baya zaidi kwa baadhi ya watu kutumia suala hilo kuiunga mkono serikali ya Marekani kuweka sera mpya za kuipinga China.

    Mtaalamu mwingine wa teknolojia ya chip wa Marekani amesema kuweka chip kwenye kompyuta ni "vitendo vya ngazi ya chini" ambavyo vinaweza kugunduliwa kirahisi, kwa hivyo hakuna nchi yoyote inayotumia njia hii kupata taarifa za kijasusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako