• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utatuzi wa mgogoro unaotokana na matumizi mabaya ya maliasili wahitaji mfumo wa maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2018-10-17 18:33:32

    Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amesema, utatuzi wa mgogoro unaotokana na matumizi mabaya ya maliasili unahitaji kuboresha matumizi ya maliasili na kusaidia nchi husika kupata maendeleo yenye uwiano ili kuingia kwenye njia ya maendeleo endelevu.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu nafasi ya matumizi ya maliasili kwenye kulinda amani na utulivu duniani, balozi Ma amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu mamlaka ya kila nchi ya kumiliki maliasili zao. Amesema nchi zinazokabiliwa na mapigano zinapaswa kuzingatia zaidi matumizi na usimamizi wa maliasili na kuepuka uchimbaji haramu wa madini ili kuwawezesha watu wote kupata manufaa kutoka matumizi mazuri ya maliasili.

    Balozi Ma amesistiza kuwa, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanatakiwa kuongeza uratibu na kusaidia nchi hizo kuongeza usimamizi wa maliasili, na kwamba China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuongeza kazi za maliasili katika kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako