• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa China katika nchi za nje waongezeka katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-10-17 19:12:41

    Takwimu kutoka wizara ya biashara ya China zimeonesha kuwa, katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu, uwekezaji wa China katika nchi za nje umeendelea kuongezeka, thamani ya uwekezaji imefikia dola bilioni 82.02 za kimarekani, ambayo imeongezeka kwa asilimia 5.1, huku uwekezaji mpya wa kampuni za China katika nchi za "Ukanda Mmoja na Njia Moja" umeongezeka kwa asilimia 12.3 ikilinganishwa na wa mwaka jana.

    Balozi mdogo wa biashara wa idara ya uwekezaji kwa nje na ushirikiano wa kiuchumi iliyo chini ya wizara ya biashara ya China Bw. Han Yong amesema, wakati China ikihimiza ujenzi wa eneo la biashara huria la ndani huko Hainan, pia itashughulikia ujenzi wa maeneo ya ushirikiano wa uchumi na biashara katika nchi za nje. Bw. Han amesema, hadi kufikia mwezi wa Septemba mwaka huu, kampuni za China zimejenga maeneo 113 ya ushirikiano wa uchumi na biashara katika nchi 46, huku zikiwekeza dola bilioni 36.63 za kimarekani. Idadi ya kampuni zilizoingia katika maeneo hayo imefikia 4,663 ambayo thamani za uzalishaji zimefikia dola bilioni 111.71 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako