• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya kupunguza gharama za biashara kwa bishara ndogo na za kadri

    (GMT+08:00) 2018-10-17 19:48:46

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jana alisema kwamba Serikali yake itawianisha michakato ili kutoa usaidizi unaostahili kwa sekta ya biashara ndogo na za kadri (SMEs).

    Akizungumza katika chuo cha Mafunzo ya Biashara cha Strathmore alipohudhuria kongamano kuhusu ukuaji wa sekta ndogo ya biashara za kadri ,Rais Kenyatta alisema kuwa sekta ya biashara ndogo na kadri inawakilisha asilimia 75 ya wafanyakazi nchini Kenya na hivyo serikali inafaa kuandaa kikao kufahamu jinsi ya kushughulikia sekta hiyo.

    Aidha alisema sekta hiyo inachangia kwa kiwango kikubwa pato la taifa (GDP).

    Rais alisisitiza kwamba serikali ya Taifa na zile za kaunti zinastahili kumarisha viwango vya usaidizi kwa sekta ya biashara ndogo na za kati.

    Na kuhusu gharama za kufanya biashara nchini Kenya,Rais Kenyatta alimuamuru Waziri wa Nishati Charles Keter kuchunguza upya gharama za nishati kwa sekta ya biashara ndogo na kadri.

    Rais alimuamuru Waziri wa Nishati kuchunguza upya gharama ya umeme katika muda wa mwezi mmoja na kuweka mpango endelevu kuhakikisha gharama ya nishati kwa sekta ndogo ya biashara za kadri imepunguzwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako