• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema hali ya mlipuko wa Ebola nchini DRC haijakuwa dharura ya kiafya duniani

    (GMT+08:00) 2018-10-18 10:01:14

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema hali ya mlipuko wa homa ya Ebola ya hivi sasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC haijafikia kuwa hali ya dharura ya kiafya duniani.

    WHO imeitisha mkutano wa kamati ya dharura kuhusu hali ya mlipuko wa Ebola nchini DRC, na kutoa hitimisho kwamba hali hiyo kwa sasa bado haijafikia kuwa hali ya dharura kwa afya ya umma duniani. Hata hivyo, shirika hilo linaendelea kufuatilia kwa makini hali hiyo, na kusisitiza kuwa macho zaidi na kuimarisha kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huo.

    Kamati hiyo imesema mlipuko huo wa homa ya Ebola umetokea kwenye eneo linalokumbwa na mapambano na msukosuko wa kibinadamu kwa muda mrefu. Imependekeza kuwa serikali ya mkoa, WHO na wadau wengine, ni lazima waimarishe operesheni zao kwa kufuatilia usalama wa watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako