• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wachina wanaotalii nchini Kenya katika msimu wa utalii wa mwaka huu yaongezeka kwa asilimia 15

    (GMT+08:00) 2018-10-18 18:28:35

    Takwimu zilizotolewa na shirika la utalii la China nchini Kenya zimeonesha kuwa, katika msimu wa utalii wa mwaka huu, idadi ya wachina waliotalii nchini Kenya imeongezeka kwa asilimia 15.

    Takwimu hizo pia zimeonesha kuwa mwaka jana, idadi ya watalii wa kigeni waliokwenda nchini Kenya ilifikia milioni 1.47. Marekani na Uingereza zimechukua nafasi mbili za mwanzo kwa idadi ya watalii zaidi ya laki moja, huku China ikichukua nafasi ya tano kwa idadi ya watlii elfu 69.

    Waziri wa utalii wa Kenya Bw. Najib Balala hivi karibuni amesema, mwaka huu pato la utalii wa Kenya linatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 15 na soko linalojitokeza kiuchumi ikiwemo China litakuwa nchi zinazowekwa kipaumbele.

    Pia amesema, mwaka jana wachina elfu 69 walitalii nchini Kenya, katika miaka miwili ijayo idadi hiyo inatarajiwa kufikia laki 1. Amesema nchi hiyo sasa inazingatia zaidi katika soko linalojitokeza kiuchumi, ikiwemo India, China hata Ulaya ya Kati na Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako